2 Chronicles 4:12-16

12zile nguzo mbili;
yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo,
zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo;
13 ayale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);
14 bvishikio pamoja na masinia yake;
15hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake;
16pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana.

Vitu vyote ambavyo Huramu-Abi alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa.
Copyright information for SwhNEN